Parimatch yaleta Chomoka na Ndinga Kombe la Dunia

24Nov 2022
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Parimatch yaleta Chomoka na Ndinga Kombe la Dunia

HUKU utamu wa michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar, Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Parimatch Tanzania imewapa wateja na wadau wake nafasi ya kubeti mchongo wa kujishindia gari mpya na ya kisasa, simu janja pamoja na bodaboda kutoka katika kampeni yao ya Chomoka na Ndinga. 

 

Hayo yalibainishwa jana na Ofisa Habari wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed, wakati alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo na kusema promosheni hiyo ni mahususi kwa wateja wao wote wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi hichi cha Kombe la Dunia. 

“Katika kipindi cha kuanzia Novemba 22 hadi 26, mwaka huu, mteja wa Parimatch akifanya bashiri kwenye mchezo wowote basi ataingia moja kwa moja katika droo ya kuwania gari aina ya Urban Cruiser yenye O kilometa kutoka katika showroom ya Toyota Tanzania, bodaboda aina ya Hero Hunter 125cc na smartphone aina ya Samsung Galaxy A03 Core (Simu janja),” alisema Mohamed. 

Aliongeza kila siku watakuwa wanatoa simu mbili na washindi watatangazwa kupitia kurasa zao za kijamii na zawadi ya bodaboda itatolewa kwa wiki mara moja, siku ya Ijumaa, kupitia droo itakayoruka kituo cha ITV, wiki husika. 

Zawadi ya gari itatolewa mwisho wa mashindano haya Desemba 27, mwaka huu ambapo droo kubwa ya kutafuta mshindi wa gari itafanyika siku hiyo. 

Pamoja na hayo, Mohamed alifafanua katika promosheni hiyo sehemu ya michezo ya TVBET, Live Casino, Casino New na michezo ya Virtual haitaruhusiwa kushiriki katika promosheni hiyo. 

Kampuni ya Parimatch imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya asilimia 100 mpaka Sh. milioni moja kwa wateja wapya wanaojiunga nao na imekuwapo nchini tangu mwaka 2019, ikitoa huduma zinazojumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. 

Mbali na soka, Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, kikapu, kriketi, baseball na michezo mingine ya Live na pre-match. 

 

 

Habari Kubwa