Pluijm: Azam kwa kukaba hawajambo

06Mar 2016
Lasteck Alfred
Lete Raha
Pluijm: Azam kwa kukaba hawajambo

KOCHA wa Yanga, Hans van der Pluijm amedai kuwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa sasa hajaona timu inayoizidi Azam kwa kucheza mpira wa kibabe.

Kocha huyo Mholanzi alisema hayo jana baada ya mchezo wa Azam na Yanga ulioisha kwa sare ya bao 2-2 kwenye mchezo uliocheza kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Pluijm alisema," kwenye mchezo wetu na Azam tulipata nafasi kadhaa tukashindwa kuzitumia lakini ugumu kwenye mchezo tuliupata kwa Azam kwa kuwa walikuwa wakicheza mpira wa nguvu.

"Kawaida kwa siku za hivi karibuni.si mchezo wa Simba, Coastal au timu nyingine. Azam wamekuwa ndio timu ngumu zaidi kwetu kwa miaka ya karibuni kutokana na kucheza la nguvu.

" Azam wanatumia nguvu na soka lao limekuwa na ubabe ambao naona kama mbinu yao ya mchezo ambayo inaweza kuwapa matokeo,"alisema kocha huyo.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Azam, Denis Kitambi alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu lakini kilichowagharimu ni maamuzi tata ya waamuzi.

" Huu ni mchezo wa nne wa ligi tunacheza dhidi ya Yanga na waamuzi wamekuwa hawatutendei haki.
"Tumeamua kulisema kwani tumekuwa hatutendewi haku.mchezo na Yanga tulistahili kushinda bao 3- 2 kwani tulipata penalti lakini tulinyimwa, " alisema.

Habari Kubwa