Polisi Morogoro waanza kujifua

27Jun 2016
Christina Haule
Morogoro
Nipashe
Polisi Morogoro waanza kujifua

TIMU ya Polisi Morogoro imeanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Daraja la Kwanza unaotarajia kufanyika kuanzia Agosti mwaka huu imeelezwa.

TIMU ya Polisi Morogoro

Mlezi wa timu hiyo, ambaye pia ni Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ulrich Matei aliliambia gazeti hili kuwa wachezaji wote wako katika hali nzuri na wanaendelea na mazoezi kama ilivyopangwa na benchi la ufundi.

Kamanda Matei alisema licha ya wachezaji hao kuwa katika hali nzuri, Kocha Mkuu wa timu hiyo John Tamba anatarajia kusajili wachezaji wengine wapya kwa lengo la kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

"Timu yetu ilianza rasmi mazoezi tangu Jumatatu (Juni 20 mwaka huu), ila tuko katika mipango ya kusajili wachezaji wengine wapya baada ya dirisha la usajili kufunguliwa rasmi na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania)," alisema Matei.

Aliongeza kuwa uamuzi wa kusajili wachezaji wapya ni kuhakikisha wanatimiza lengo lao la kupanda daraja na kurejea kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

www.guardian.co.tz/circulation