Prisons yaitisha Ruvu Shooting

18Mar 2023
Adam Fungamwango
MBEYA
Nipashe
Prisons yaitisha Ruvu Shooting

KLABU ya Prisons imesema mechi dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa Aprili 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya ndiyo itaanza kuamua hatima yao ya kubaki katika Ligi Kuu au kushuka daraja, imeelezwa.

 

Ofisa Habari wa Prisons, Jackson Mwafulango, alisema jana wameandaa mikakati kabambe ya kuhakikisha wanashinda mechi hiyo.

Mwafulango alisema wanajua Ruvu Shooting haipo katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi, lakini watawasamehe kwa sababu nao wapo kwenye mkakati wa kuhakikisha timu yao inabaki Ligi Kuu.

"Prisons ni moja ya timu nzuri, lakini upepo mbaya ulipita kati na sasa timu inaonekana imekaa vyema, tunamheshimu Kocha Mbwana Makata na benchi lake la ufundi, tunaiheshimu Ruvu Shooting kama timu nzuri iliyokamilika ndani ya nje ya uwanja, lakini watatusamehe kwa sababu tunajua tukishinda mechi hiyo, itaturahisishia kazi kuelekea mechi zinazofuata," alisema kiongozi huyo.

Hata hivyo alimsifu Kocha, Abdallah Mohamed 'Bares' kwa kuibadilisha timu hiyo ambayo sasa imerejesha matumaini ya kusalia katika Ligi Kuu Bara.

 

Habari Kubwa