Pwani waungana kuikoa JKT Ruvu

16Mar 2016
Somoe Ng'itu
Tanga
Nipashe
Pwani waungana kuikoa JKT Ruvu

WADAU wa soka wa mkoa wa Pwani wameungana na uongozi wa JKT Ruvu Stras kuhakikisha timu hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara haiporomoki daraja msimu huu.

Hassan Othman 'Hassanoo', kulia akiwa na Ismail Aden Rage.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Pwani, Hassan Othman 'Hassanoo', aliambia Nipashe jana kuwa wamekutaka na kupanga mikakati mbalimbali ili timu hiyo ifanye vizuri katika mechi zake zilizobaki kabla ya kumalizika kwa msimu huu Mei 7.

Hassanoo alisema hatua ya kwanza ilikuwa ni kuirudisha kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani humo na wanalishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukubali ombi hilo.

"Hatutakubali kuona timu yetu inashuka daraja, mkakati wa kwanza ulikuwa ni kuona Ruvu Shooting inarejea na umekamilika, sasa tunapambana usiku na mchana kuhakikisha JKT Ruvu haishuki daraja," alisema Hassanoo.

Baada ya kurejea Mabatini kutoka kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, JKT Ruvu inayofundishwa na Abdallah 'King' Kibadeni, imeshinda mechi mbili nyumbani dhidi ya Toto Africans (2-0) na Mwadui FC (1-0).

Timu hiyo sasa iko katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na mtaji wa pointi 21 baada ya mechi 23 na ina mechi mbili za nyumbani dhidi ya Ndanda FC na Stand United.

Habari Kubwa