Real Madrid sasa waamua kumgeukia Lewandowski

10Sep 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Real Madrid sasa waamua kumgeukia Lewandowski
  • ***Nia kama watashindwa kumsajili straika wa kimataifa wa Norway, Haaland kutoka Dortmund ambaye...

REAL Madrid inapanga kumsajili Robert Lewandowski kutoka Bayern Munich kama watashindwa kumchukua Erling Haaland kutoka Borussia Dortmund, kwa mujibu wa AS.

Straika huyo wa Dortmund, Haaland ni mmoja wa wachezaji wanaowaniwa sana na Madrid, lakini kama watashindwa kumsajili raia huyo wa Norway, watahamia kwa nyota wa kimataifa wa Poland, Lewandowski.

Lewandowski mwenye umri wa miaka 33, tayari amefunga mabao matano katika mechi tatu za Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga, msimu huu.

Kwa kipindi cha msimu wa 2020-21, straika huyo alifunga mabao 41 kwenye ligi na kutoa mchango katika mabao saba.

Msimu wa 2019-20, mchezaji huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alifunga mabao 34 na kutoa 'asisti' nne kwenye ligi.

Haaland mwenye umri wa miaka 21, amefunga mabao 27 na kutoa asisti sita kwenye Bundesliga, na kufunga mabao 10 na kutoa asisti mbili kwenye mechi nane za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Haaland pia amekuwa akihusishwa pia na Manchester City, Manchester United, Paris Saint-Germain, Juventus, Liverpool, Barcelona na Bayern Munich.

Madrid pia kwa muda mrefu wamekuwa wakihusishwa na nyota wa PSG, Kylian Mbappe.

Mbappe amekataa kuongeza mkataba mpya na PSG na hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu ujao.