Riadha wakwama kuingia kambini

05Apr 2016
Dar
Nipashe
Riadha wakwama kuingia kambini

TIMU ya taifa ya riadha imeshindwa kuingia kambini kujiandaa na michuano ya Afrika Mashariki kutokana na ukata.

Timu hiyo ilikuwa ikihitaji kiasi cha Sh. milioni 44 ili iweze kujiandaa na michuano huyo ambayo Tanzania atakuwa mwenyeji.

wanariadha hao walipangwa kuanza mapema mwezi huu mjini Morogoro, lakini hadi sasa kambi hiyo imeshindwa kuanza kutokana na kukosa fedha.

Akizungumza na gazeti hili jana Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Omben Zavalla alisema pia kuwa hawajapata kiasi cha Sh. milioni 72 kama mwenyeji wa mashindano.

Alisema bila ya wadhamini kujitokeza kusaidia timu hiyo inaweza isiingie kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo.

Kuhusu timu shiriki, alisema tayari wameshazitumia barua za kuzialika kuja kwenye mashindano hayo yenye lengo la kuibua vipaji

Habari Kubwa