Ronei afuta ukimya Bongo Fleva

06Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Ronei afuta ukimya Bongo Fleva

MSANII wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’, Rojars Elias, ‘Ronei’ amesema ukimya wake katika fani hiyo haumaanishi ameachana na muziki, ila anausoma kwanza ushindani sokoni.

Akizungumza jijini Dar ses Salaam jana, Ronei alisema muziki kwa sasa unachangamoto na mashabiki wanataka muziki mzuri na wenye ubora hivyo ukimya wake ni wa kujipanga kwa ajili ya kuachia kazi inayokubalika.

Ronei, alisema baada ya kimya hicho cha muda mrefu, tayari ameachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Dalili’.“Video ya wimbo huu mpya nategemea kuiachia ndani ya kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa, ni video itakayokuwa na ubora mkubwa,” alisema Ronei.

"Sikuwa na haraka, nilikuwa najipanga kuliteka soko la muziki ndio maana nimeachana na kufanya kolabo na kuamua kuja na nyimbo yangu mpya ya dalili ambayo inahusiana na mapenzi, ninaamini mashabiki wangu wataipenda," alisema Ronei

Aidha, alisema kulingana na ushindani uliopo katika soko la muziki ni kwamba amejipanga vizuri chini ya meneja wake ili kipaji chake kiweze kujulikana kupitia kazi zake.