Rose Muhando, Msama wakorogana

29Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Mwanza
Nipashe
Rose Muhando, Msama wakorogana

MUIMBAJI mahiri wa nyimbo za Injili nchini na Afrika Mashariki, Rose Muhando, amemuacha ‘solemba’ Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama, Alex Msama baada ya kushindwa kuhudhuria Tamasha la Pasaka katika mikoa ya Geita, Mwanza na Kahama mkoani Shinyanga.

Rose Muhando.

Kutokana na kushindwa kushiriki tamasha hilo, mkurugezi wa kampuni hiyo, Msama alisema anafutaka rasmi mkataba na msanii huyo.

“Sitafanya kazi tena na Muhando (Rose), nimekata mkataba na kampuni yangu," alisema Msama na kuongeza: "Nilimlipa kila kitu kwa ajili ya tamasha hili na pia kumtumia gari hadi Dodoma ili aweze kwenda Geita na Mwanza, lakini alimgandisha nje dereva wangu kwa muda mrefu,” alisema Msama.

Hata hivyo, Nipashe ilipomtafuta Muhando (Rose) kwa ajili ya kukatishwa ‘ghafla’ mkataba wake na Msama, hakuweza kupatikana kutokana na simu yake ya mkono kutokuwa hewani.

Habari Kubwa