Ruvu shooting walia na bahati

12Nov 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Ruvu shooting walia na bahati

KOCHA wa Ruvu Shooting, Seleman Mpungwe, amesema kuwa wapinzani wao katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga walikuwa na bahati kuondoka pointi tatu.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Yanga ikitoka nyuma ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Akizungumza na baada ya mchezo huo, Mpungwe alisema kuwa timu yake ilikuwa na nafasi kubwa kuondoka na pointi lakini umakini mbovu wa washambuliaji wake waliwagharimu.

"Nafikiri tulicheza vizuri zaidi ya Yanga na tulijitahidi kutengeneza nafasi lakini wenzetu ni kama walikuwa na bahati," alisema Mpungwe.

Aidha, alisema kuwa maamuzi ya mwamuzi wa kati wa mchezo huo Mathew Akrama, yaliwaminya muda mwingi wa mchezo.

"Tumemaliza mechi zetu za mzunguko wa kwanza tunaenda kujipanga kwa ajili ya mzunguko wa pili..., lakini ni vizuri malalamiko ya timu kwa waamuzi yafanyiwe kazi," alisema Mpungwe

Katika mchezo huo, Ruvu Shooting ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli la mapema (dakika ya saba) lakini magoli na Simon Msuva na Haruna Niyonzima yalitosha kuipa Yanga pointi tatu muhimu.

Habari Kubwa