Rwakatare afundwa akishinda Urais OBFT

03Dec 2018
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Rwakatare afundwa akishinda Urais OBFT

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT), limewataka viongozi wapya wa Shirikisho la Ngumi za Wazi (OBFT), kuacha kuokoteza mabondia wa timu ya Taifa kupitia Dar es Salaam peke yake na badala yake watoke kwenda mkoani kutafuta vipaji.

Katibu wa BMT, Alex Nkenyenge ndiye aliyetoa rai hiyo wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa baraza hilo.

 

Viongozi waliochaguliwa ni Rais Muta Rwakatare, ambaye amepata kura (13), na kumshinda wapinzani wake Yono Kevela aliyepata kura 12, huku Samweli Samwel akipata kura nane.

 

Nafasi ya Makamu wa Rais imekwenda kwa Andrew Muhoja mgombea pekee baada ya mpinzani wake kukatwa. Muhoja alipata kura 29, huku kura mbili zikiharibika, wakati Katibu Mkuu, Lukelo Wililo alichaguliwa kwa kura 23.

 

Kwa upande wa wajumbe waliochaguliwa ni Scolastika Levels (kura 25), Riadha Kimweli (kura 29), Mafuru Mafuru (kura 23), Mohamed Aboubakary (kura 27) na Zainabu Mbonde (kura 24).

 

Akizungumza baada ya kuchaguliwa Rais wa OBFT, Rwakatare alisema kwa kuanza shirikisho hilo litapeleka mashindano ya ngumi Iringa ambayo yatakutanisha timu za mabondia kutoka mikoa mbali mbali ili kupata vipaji.

 

 

Habari Kubwa