Samatta alivyofunika dakika 17 Genk

08Feb 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Samatta alivyofunika dakika 17 Genk

MBWANA Samatta juzi alianza kuandika historia yake ya kucheza soka la kulipwa Ulaya baada ya kucheza kwa dakika 17 akiwa na timu yake mpya ya KRC Genk ya Ugiriki iliyoshinda bao 1-0 katika mechi ya ligi kuu nchini huo.

KRC Genk ilifunga bao hilo pekee dhidi ya Mouscron- Peruwetz katika dakika ya 62 kupitia kwa Buffel na kuipandisha timu hiyo hadi nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 38.

Katika mechi hiyo, Samatta mshindi wa tuzo ya tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika aliingia akichukua nafasi ya Nikos Karelis.

Kabla ya hapo, Samatta alipewa nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi cha akiba kabla ya kupelekwa kikosi cha kwanza.

"Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru Watanzania pamoja na mashabiki wangu wote wa KRC- Genk kwa maombi na leo (juzi) nimefanikiwa kucheza mchezo wa rasmi nikiwa na klabu yangu mpya ya KRC-Genk na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0," aliandia Samatta katika ukurasa wake wa Instagram usiku wa kuamkia jana.

Samatta alijiunga na timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1988 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo aliichezea kwa muda wa miaka minne kuanzia mwaka 2011.

Mshambuliaji huyo aliyezaliwa 1992 alisaini mkataba wa miaka minne baada ya TP Mazembe kukubali kumuuza kwa dau la Euro 800,000.

Habari Kubwa