Samatta atangaza vita kuipeleka Stars Afcon

20Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Samatta atangaza vita kuipeleka Stars Afcon

NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta, amesema Tanzania ina nafasi ya kucheza fainali za Afrika kama kila mmoja atapambana ipasavyo kwenye mchezo dhidi ya Uganda Jumapili.

NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta, picha mtandao

Stars itashuka Uwanja wa Taifa Jumapili kuivaa Uganda ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ugenini walipokutana na timu hiyo inayoongoza msimamo wa Kundi L ambayo pia tayari ina tiketi mkononi ya kushiriki Afcon Juni mwaka huu nchini Misri.

Samatta ambaye amewasili nchini juzi akitokea Ubelgiji kwa ajili ya mchezo huo, alisema kama wachezaji watapambana uwanjani kuhakikisha wanapata ushindi kwenye uwanja wa nyumbani.

"Hii ni mechi muhimu sana kwetu..., kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo huu..., mimi naamini kama tutapambana dakika zote tunaweza kufanya vizuri," alisema Samatta.

Aidha, aliwataka mashabiki na Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwasapoti kwenye mchezo huo muhimu.

Katika kundi lao, Stars ina pointi tano sawa na Lesotho, huku Cape Verde ikiburuza mkia kwa alama zake nne.

Uganda tayari imefuzu kushiriki fainali hizo na kuzifanya Tanzania, Cape Verde na Lesotho kuwania nafasi moja kuungana nayo.

Habari Kubwa