Samia aipongeza tumu ya vijana U-23 kwa kuibuka washindi CECAFA-2021

01Aug 2021
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Samia aipongeza tumu ya vijana U-23 kwa kuibuka washindi CECAFA-2021

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameipongeza timu ya vijana chini ya miaka 23 kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA-2021).

Rais Samia ametoa pongezi hizo leo Agosti 1, katika ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika :-

“Nawapongeza timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 23 kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA-2021). Ushindi huu ni heshima kwa nchi yetu na ni chachu ya kukuza michezo. Natoa wito kwa wadau wa michezo kuendeleza jitihada za kukuza michezo yetu.”