Serengeti Boys yaahidi makubwa

12May 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Serengeti Boys yaahidi makubwa

KIKOSI cha timu ya soka ya vijana ya umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kiliondoka nchini jana kuelekea India kwa ajili ya kushiriki mashindano maalum ya kimataifa yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Jumamosi.

serengeti boys

Yosso hao watashuka uwanjani Jumapili kucheza mechi yao ya kwanza dhidi ya Marekani itakayofanyika kwenye Uwanja wa Tilak Maidan, Vasco, Goa.

Mkuu wa msafara wa timu hiyo na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi alisema jana kuwa wachezaji wote wako katika hali nzuri na wanaahidi watapeperusha vyema bendera ya nchi.

"Tuko ndani ya ndege tunatarajia kuanza safari muda si mrefu, tunashukuru kuipata nafasi hii kwa sababu itawapa mazoezi mazuri wachezaji wetu," alisema Nyenzi jana 9:20 mchana.

Nyenzi alisema kuwa wanatarajia kutumia mechi hizo kupata uzoefu na kujiweka imara na mchezo wao dhidi ya yosso wa Shelisheli utakaofanyika Juni mwaka huu.

Habari Kubwa