Akizungumza jana wakati alipoitembelea timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura, alisema wanahitaji kuwa na usimamizi unaoeleweka wa kusimamia mapato.
Wambura alisema kuwa baada ya kukamilika kwa mfumo huo, serikali pia itajipanga namna ya kuisaidia Twiga Stars katika mechi zake badala ya kuacha kukata kodi katika mapato ambayo timu hiyo itaingiza.
"Tunahitaji kuwa na usimamizi mzuri, hadi sasa hesabu zilizopo na idadi ya viti vilivyopo bado jambo hili linatutia shaka, mapato halisi hayajapatikana, suluhisho hapa ni tiketi za kielektroniki," alisema Naibu Waziri huyo.
Hata hivyo, Wambura bila kusema ni msaada gani watautoa kwa Twiga Stars ambayo iko kambini kwa ajili ya kujiandaa kuikabili Zimbabwe Machi 4 mwaka huu, alisema Serikali kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watahakikisha mambo yanakwenda vizuri kwenye timu hiyo.
Aliwataka wachezaji wa Twiga Stars kutokata tamaa ya kujituma zaidi licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali wakati wa maandalizi yao