Shabiki wa Madrid Ifakara ashinda milioni 208/-

21May 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Shabiki wa Madrid Ifakara ashinda milioni 208/-

SHABIKI wa timu ya Real Madrid na mkazi wa Ifakara, mkoani Morogoro, Gadi Mwajeka ameibuka mshindi wa zawadi ya Sh. milioni 208. 5 baada ya kubashiri kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 wa Kampuni ya M-Bet.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani hiyo,  Mwajeka alisema hakuamini mara baada ya kupigiwa simu kuambiwa yeye ndiye mshindi wa zawadi hiyo ya fedha.

Mwajeka ambaye ni mfanyabiashara ya rangi za mkeka katika eneo la Ifakara mjini, alisema ushindi huo ni faraja kubwa sana kwake na anaamini utamsaidia kuboresha biashara yake na vile vile kaunzisha nyingine mpya.

Sikuamini kama nimeshinda kiasi kikubwa cha fedha, nimetumia kiasi cha Sh. 1,000 tu kubashiri na kuingiza kiasi kikubwa cha fedha. Nimefarijika sana, alisema Mwajeka.

Alisema ameshiriki kubashiri kwa muda wa miaka mitatu na mwaka huu ndio amebahatika kuibuka kinara wa kiasi hicho kikubwa cha fedha.

"Mke wangu ni nesi, nilikuwa nachukua madaftari yake kuandika timu na kuanza kuzipigia mahesabu. Nitatumia fedha hizi kwa ushauri wa wazazi wangu kuona ninafanya biashara gani," alisema.

Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi, alisema Mwajeka ni mshindi wao wa tano kushinda zawadi hiyo nono, tangu walipoanza shindano hilo mapema mwaka huu.

Mushi alisema M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwaomba mashabiki wa soka kubashiri na kampuni yao ili kuweza kubadili maisha yao.

M-Bet ni nyumba za mabingwa na mabingwa wote wanapatikana kupitia michezo ya kubahatisha ya kampuni yetu, kujitajirisha vilevile kuichangia nchi yao kwani asilimia 20 ya fedha hukatwa kama kodi ya kusaidia maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali, aliongeza Mushi.

Habari Kubwa