Shime: Serengeti Boys itafuzu Afrika

09Aug 2016
Faustine Feliciane
Dar es Salaam
Nipashe
Shime: Serengeti Boys itafuzu Afrika

KOCHA wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Bakari Shime, amesema kuwa hatua waliyofikia wana nafasi kubwa ya kufuzu kwa fainali za Afrika za Vijana zitakazofanyika mwakani Madagascar.

Bakari Shime.

Kikosi cha Serengeti Boys, juzi kililazimisha sare ugenini dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali hizo.

Akizungumza jana,Shime alisema matokeo waliyoyapata juzi dhidi ya Afrika Kusini yatawpa chachu ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini Dar es Salaam.

"Kwa sasa akili zatu tunapeleka kwenye mchezo wetu wa marudiano, tumebakisha hatua chache kufuzu,tutapambana kwenye mchezo huo,"alisema Shime.

Serengeti Boys inahitaji ushindi wowote kwenye mchezo huo wa marudiano utakaochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi ili ifuzu kwa fainli hizo za Afrika kwa vijana.