'Simba ina dakika 180 za kuimaliza Yanga'

07Feb 2016
Nipashe Jumapili
'Simba ina dakika 180 za kuimaliza Yanga'

NI Kama vile kocha na wachezaji wa Simba wamepania kotoa kipigo cha kisasi dhidi ya watani wao Yanga katika mchezo baina yao -- Ligi Kuu Bara Februari 20 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha wa Simba, Jackson Mayanja alisema anaamini wapinzani wao wanafungika kama ilivyo kwa timu nyingine wanazokutana nazo katika michuano hiyo.
"Ushindi dhidi ya Yanga utategemeana na michezo miwili ya ligi -- dhidi ya Kagera Sugar na Stand United tutakayoicheza ndani ya siku saba.
“Natambua kuwa mashabiki wengi wanangoja kwa hamu mchezo wa Simba na Yanga. Nafahamu umuhimu wa mchezo huo.
“Kuna mambo ambayo ninayatazama kwa umakini kwenye michezo miwili ijayo (wa leo na Kagera na ule wa Stand) na matokeo nitakayoyapata ndiyo yatakayonionyesha mbinu za kuifunga Yanga.
“Ninaendelea kuwatengenezea wachezaji mifumo rafiki lakini pia stamina ambayo itawawezesha kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa.
“Ushindi ndiyo lengo letu kubwa na wachezaji wananielewa vizuri. Kwa sasa naendelea kuisoma Yanga kadri niwezavyo na wachezaji wangu watafanya vizuri."
Mara ya mwisho Yanga ilikutana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Septemba 26 mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa na Simba kulala kwa mabao 2-0 ikiwa chini ya kocha aliyetimuliwa Dylan Kerr.

Habari Kubwa