Simba kamili kuivaa Stand

01Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Simba kamili kuivaa Stand

LICHA ya mchezo wao na Stand United kurudishwa nyumba kwa siku mbili, Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema kikosi chake kiko tayari kuwavaa wageni hao kutoka Shinyanga.

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma

Akizungumza na gazeti hili jana, Djuma, alisema kuwa wamejipanga kucheza kwa juhudi katika mchezo huo ili waweze kukusanya pointi tatu muhimu na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Djuma alisema kuwa anajua Stand United pia wamekuja Dar es Salaam kutafuta ushindi, hivyo wamejipanga kukabiliana na ushindani watakaokutana nao katika mchezo huo.

"Tumepata taarifa ya mabadiliko ya mechi, tuko tayari kwa mchezo huo na tunaamini hautakuwa mchezo rahisi, mechi zote za ligi ni ngumu na tunawaandaa wachezaji wetu kupambana, bado vita ya ushindani ni kubwa," alisema kocha huyo anayesaidiana na Mfaransa, Pierre Lechantre.