Simba na leo tena

15Oct 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Simba na leo tena

VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC wanatarajiwa kushuka dimbani leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kumenyana na Kagera Sugar ya Bukoba.

Shizza Kichuya.

Simba wanaingia kwenye mchezo huo wakitoka kushinda mechi ya ugenini dhidi ya wenyeji Mbeya City Jumatano Uwanja wa Sokoine, mabao 2-0 wafungaji Ibrahim Hajib na Shizza Kichuya.

Mchezo huo namba 73, unatarajiwa kuchezeshwa na refa Hussein Athumani kutoka mkoani Katavi, ambaye atasaidiwa na Joseph Bulali wa Tanga na Sylvester Mwanga wa mkoani Kilimanjaro wakati Soud Lila wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba huku Kamishna wa mchezo akiwa Pius Mashera wa Dodoma.

Mchezo mwingine namba74 kati ya JKT Ruvu na Mwadui ya Shinyanga utafayika Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani ambao utachezeshwa na Mwanamama mwenye beji la FIFA, Mwanahamisi Matiku, atakayesaidiwa na Shaffi Mohamed wote wa Dar es Salaam na Gesper Ketto wa Arusha.

Mwamuzi wa akiba atakuwa Abdallah Rashid wa Pwani wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Charles Mchau wa Kilimanjaro.

Stand United ya Shinyanya itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kambarage katika mchezo namba 75 ambao utachezeshwa na Eric Onoka wa Arusha akisaidiwa na Agnes Pantaleo pia wa Arusha na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Joseph Pombe wa Shinyanga.

Kamishna wa mchezo atakuwa Hamisi Kitila wa Singida.

Ligi hiyo itaendelea keshokutwa Jumapili kwa mchezo namba 76 utakaozikutanisha timu za Azam na Yanga SC zote za Dar es Salaam utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, ukichezeshwa Israel Nkongo wa Dar es Salaam pia, atakayesaidiwa na Soud Lila na Frank Komba na mwamuzi wa akiba atakuwa Helen Mduma; wote wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Michael Wambura pia wa Dar es Salaam.

Mchezo namba 77 utazikutanisha timu za Ruvu Shooting na Mbeya City Jumapili Oktoba 16, 2016 kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa Rudovic Charles wa Tabora akisaidiwa na Samwel Mpenzu wa Arusha na Jeremina Simon wa Dar es Salaam. Kamisha wa mchezo huo atakuwa Idelfonce Magali wa Morogoro.

Mtibwa Sugar ya Morogoro na Tanzania Prisons ya Mbeya nazo zitacheza Jumapili Oktoba 16 kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro. Mchezo huo namba 78 utachezeshwa na Elly Sasii wa Dar es Salaam.

Waamuzi wasaidizi ni Ferdinand Chacha wa Mwanza Lulu Mushi wa Dar s Salaam wakati mwamuzi wa akiba Nicolaus Makalanga wa Morogoro. Kamishna ni George Komba wa Dodoma.

Mchezo mwingine wa Jumapili utakuwa kati ya Toto African ya Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mchezo huo Na. 79 utachezeshwa na mwamuzi Shomary Lawi wa Kagera akisaidiwa na Abdallah Uhako wa Arusha na Julius Kasitu wa Shinyanga huku mwamuzi wa akiba akiwa Mathew Akrama wa Mwanza.

Kamishna atakuwa Michael Bundala wa Dar es Salaam.

Habari Kubwa