Simba Queens yafikiria ubingwa

21May 2020
Saada Akida
Dar es Salaam
Nipashe
Simba Queens yafikiria ubingwa

KOCHA Mkuu wa Simba Queens, Mussa Hassan 'Mgosi', amesema mikakati yake ni kuona timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yake iliyobakia na hatimaye kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake kwa mara ya kwanza msimu huu.

Mgosi ameliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana mikakati aliyonayo ni kuwabadilishia wachezaji wake programu ya mazoezi ili kufidia muda ambao ligi hiyo ilisimama.

Kiungo huyo mshambuliaji wa zamani wa Simba, alisema ligi itakaporejea, timu yake itafanya mazoezi mara mbili kwa siku.

Alisema anahitaji kuleta mabadiliko katika soka la wanawake hivyo anahitaji kikosi chake kifanikishe malengo waliyonayo na kuleta mapinduzi kwenye ligi hiyo ya juu kwa wanawake hapa nchini.

"Malengo yangu ni kuleta mabadiliko katika mpira wa kike, ninahitaji sana msimu huu kuchukuwa ubingwa sababu hiyo nimekuwa karibu kuwafatilia wachezaji wangu katika kipindi hiki cha janga la corona,” alisema Mgosi.

Aliongeza ana imani na kikosi chake na hata ligi hiyo ikirejeshwa leo, hana wasiwasi na nyota wake wa Simba Queens.

Simba Queens inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 29 lakini wana michezo miwili mkononi wakati vinara ni JKT Queens ambao wamecheza mechi mbili zaidi.

Habari Kubwa