Simba Queens yaichapa Yanga

11Jul 2020
Saada Akida
Dar es Salaam
Nipashe
Simba Queens yaichapa Yanga

SIMBA Queens imeendeleza ubabe kwa watani zao baada ya kuwafunga mabao 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena.

Ushindi huo umeifanya Simba Queens kujiimarisha katika kilele cha msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 38 wakati watani zao Yanga Princess wamebakiwa na pointi 23.

Mabao ya Simba Queens katika mchezo huo yalifungwa na nahodha, Mwanahamisi Omary na Opa Clement kila mmoja alifunga magoli mawili huku lingine likiwekwa kimiani na kiungo wa kimataifa wa timu hiyo kutoka Burundi, Joelle Bukuru.

Bao la kufutia machozi la Yanga Princess katika mchezo huo wa mzunguko wa pili lilifungwa na Shelder Boniface.

Nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ambayo kila timu imecheza mechi 15 inashikiliwa na mabingwa watetezi, JKT Queens yenye pointi 35 na Ruvuma Queens inafuata ikiwa na pointi 34.

Habari Kubwa