Simba SC waenda mbio kumaliza ishu ya Mavugo

14Aug 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Simba SC waenda mbio kumaliza ishu ya Mavugo

UONGOZI wa Simba SC umesema upo katika hatua za mwisho kumaliza suala la uhamisho wa mshambuliaji wao, Laudit Mavugo.

laudit mavugo.

“Tupo katika hatua za mwisho za kushughulikia uhamisho wa Mavugo, ili ahalalishwe kuichezea timu yetu mara moja,”alisema juzi jioni Katibu wa Simba, Patrick Kahemele alipozungumza na Lete Raha mjini Dar es Salaam.

Mavugo amekuja Simba SC baada ya kumaliza Mkataba wake Vital’O ya kwao Burundi, lakini ajabu klabu hiyo imeibuka na kudai mshambuliaji huyo wa Int’amba Murugamba ana mwaka mmoja zaidi.

Vital inaitaka Simba SC mezani wazungumze biashara ya Mavugo, lakini Kahemele amesema; “Sisi hatuna suala la kuzungumza na Vital’O kuhusu Mavugo. Tunashughulikia uhamisho wake tu kwa wahusika,”.

Pamoja na hayo, klabu ya Solidarity nayo imeibua madai ya kummiliki Mavugo na kuitaka Simba SC ikao nao mezani kuzungumzia uhamisho wake.

Mavugo leo anatarajiwa kuichezea mechi ya pili Simba SC, itakapomenyana na URA ya Uganda Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mavugo alicheza vizuri katika mechi yake ya kwanza Uwanja wa Taifa Jumatatu wiki hii dhii ya AFC Leopard ya Kenya, Simba SC ikishionda 4-0, naye akifunga bao moja.

Wakati huo huo: Simba SC inatarajiwa kuwa na kikao na mfanyabiashara Mohamed ‘Mo Dewji’ kesho mjini Dar es Salaam kujadili mpango wake wa kutaka kununua asilimia 51 ya hisa za klabukwa Sh. Bilioni 20.

Kahemela alisema jana kwamba maandalizi yote ya kikao hicho kitakachofanyika katika hoteli moja kubwa Jijini yamekamilika na wamekwishamuarifu na Mo Dewji pia.

Habari Kubwa