Timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, imecheza mechi 10 ugenini hadi sasa, ikishinda mechi sita, sare tatu na kufungwa mechi moja tu.
Simba pia imevuna pointi 21 ikicheza nyumbani uwanja wa Taifa.
Kwenye msimamo wa ligi, timu hiyo inakamata nafasi ya pili kwa pointi 42 sawa na Azam, lakini ikiwa na faida ya magoli mengi ya kufunga.
Azam, ambayo inakamata nafasi ya tatu kwa pointi 42, inafuatia kwa kukusanya pointi nyingi ugenini baada ya kuvuna pointi 19.
Timu hiyo imecheza mechi saba ugenini, ikishinda sita na kutoka sare moja, huku ikivuna pointi 23 nyumbani.
Mabingwa watetezi Yanga, ambao wanaongoza ligi wakiwa na pointi 43, wanakamata nafasi ya tatu kwa kuzoa pointi nyingi ugenini.
Yanga imejikusanyia pointi 18 mikoani, ikiwa imecheza mechi tisa, ikishinda tano, sare tatu na kufungwa mechi mechi moja.
Timu hiyo ndiyo inaongoza kwa kukusanya pointi nyingi nyumbani, kwa kujizoelea pointi 25.
Mtibwa Sugar inayokamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 33, iko nafasi ya nne kwa pointi nyingi ugenini, kwani imezoa pointi 14, huku nafasi ya tano ikishikiliwa na Prisons iliyojipatia pointi 10 ikicheza nje ya Uwanja wa Sokoine Mbeya.
Timu ya Coastal Union ndiyo inayoshika mkia kwa kupata pointi chache ugenini, ambapo imekusanya mbili tu hadi sasa.