Simba wapata CEO mpya

06Sep 2020
Saada Akida
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Simba wapata CEO mpya

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohamed Dewj 'Mo' jana amemtambulisha rasmi Mtendaji Mkuu mpya wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez.

Akizungunza na waandishi wa habari jana, Mo alisema kuwa walikaa kwenye kikao cha bodi na kumteua Barbara kuziba nafasi ya aliyekuwa mtendaji mkuu wa timu hiyo, Senzo Mazingiza.

Mo alisema kuwa kutokana na vigezo pamoja na uzoefu aliokuwa nao bodi imeona ni vyema yeye akashika nafasi hiyo na anaamini atafanya vizuri.

"Tulikaa jana (juzi) kwenye kikao cha bodi na kumpendekeza Barbara kuwa mtendaji mkuu baada ya kuonyesha uwezo mkubwa pindi alipokaimu nafasi hiyo alifanya vizuri zaidi hivyo bodi ikapendekeza awe mtendaji wetu kwa sasa," alisema Mo.

Naye Mtendaji Mkuu, Barbara alisema kuwa amefurahi kupata nafasi hiyo na atahakikisha anaendeleza mazuri na mafanikio yaliyokuwepo.

"Nimefurahi kupata nafasi ya kuwa mtendaji mkuu wa Simba na nitahakikisha nashirikiana vizuri na wafanyakazi wezangu ili kuendeleza mafanikio ya klabu yetu," alisema Barbara.

Agosti 8, mwaka huu aliyekuwa mtendaji mkuu wa timu hiyo Mazingiza alijiuzuru kwenye nafasi yake na sasa ni mshauri mkuu wa timu ya Yanga.

Habari Kubwa