Simeone: Tutapambania nne bora

10May 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Simeone: Tutapambania nne bora

DIEGO Simeone amesisitiza kuwa Atletico Madrid bado wana kazi kubwa ya kufanya kama wanataka kumaliza katika nafasi nne za juu za Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Atletico waliwashinda wapinzani wao wakubwa, Real Madrid bao 1-0 wakiwa Wanda Metropolitano Jumapili na kusonga mbele kwa pointi sita dhidi ya Real Betis walio katika nafasi ya tano huku kukiwa na mechi tatu kabla ya msimu kumalizika.

Mkwaju wa penalti wa Yannick Carrasco dakika ya 40, ulitosha kwa Atletico kupata ushindi huo.

'Los Rojiblancos' hao wanaweza kufuzu kwa mara ya 10 mfululizo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kama watapata pointi tatu dhidi ya Elche Jumatano, lakini Simeone amesema wanatakiwa kupambana.

"Zimesalia mechi tatu. Kila mmoja anashindana kumaliza nafasi ya nne na haitakuwa rahisi," alisema akiiambia Movistar.
"Lakini kwa kweli hii ni hatua kali na ya maamuzi kwetu.

"Tulicheza mchezo ambao tulitaka kucheza. Tulipata nafasi nyingi, lakini hatukuweza kutumia nguvu na hilo lilitusukuma."

Habari Kubwa