SportPesa, tiGO Pesa, Airtel Money waja na 'Mshiko Deilee'

11Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
SportPesa, tiGO Pesa, Airtel Money waja na 'Mshiko Deilee'

WAKATI michuano ya Euro 2020 ikianza leo barani Ulaya, Kampuni ya Michezo na Burudani ya SportPesa, imezindua kampeni maalumu kwa ajili ya mechi zote za mwezi huu ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake.

Promosheni hiyo ambayo ilizinduliwa Masaki jijini Dar es Salaam jana, imehusisha kampuni za mitandao ya simu ya Tigo, Vodacom na Airtel, zote kwa pamoja zikiwa na lengo la kuwazawadia wateja hasa katika kipindi hiki cha michuano ya Euro 2020 na mingine inayoendelea ikiwamo Copa America na Ligi Kuu Tanzania Bara, VPL.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa, Sabrina Msuya, alisema katika kipindi hiki wameona ni vema kuwazawadia wateja wao wote kwa kuzindua promosheni hiyo ambayo inakwenda kwa jina la “Mshiko Deilee”.

Promosheni hii inaanza rasmi leo Mei 11 na kumalizika mwezi ujao tarehe 11. Kutakuwa na washindi wa kila siku ambao watajishindia kiasi cha shilingi 10,000 kila mmoja kwa watu 30, pia tutatoa shilingi milioni moja kila wiki kwa washindi watatu na mwisho wa promosheni tutatoa Sh. 15,888,000 kwa mshindi mmoja atakayebahatika.

“Droo zitachezwa kila siku na washindi watatangazwa kupitia kurasa zetu za Instagram na Facebook. Pia katika kurasa za washirika wetu ambao ni Tigo, Vodacom na Airtel, pamoja na kurasa za Klabu za Simba na Yanga,” alisema na kupongeza:

“Ili kushiriki kwenye promosheni hii ni lazima kuweka pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa, kisha kuanza kucheza ili kuingia katika droo na kupata nafasi ya kuibuka mshindi. Kwa wateja wapya watatakiwa kujisajili kwanza kisha kufuata mtiririko huo huo.

“Napenda kuwakaribisha watumiaji wa mitandao yote kushiriki kwenye promosheni hii hata wale ambao hawajajisajili na SportPesa ili waweze kushinda zawadi za kila siku, kila wiki na zawadi kubwa kabisa ya zaidi ya shilingi milioni 15”.

Kwa upande wa Meneja Biashara wa Tigo Pesa, Fabian Felician, alisema: “Katika msimu huu wa mechi za Euro na zinginezo tumeona ni vizuri kushirikiana na washirika wetu SportPesa ili wateja wetu wa Tigo Pesa waweze kubashiri kwa urahisi na kupata nafasi ya kujishindia mamilioni ya pesa.

Alisema kushiriki ni rahisi, kwani mteja wa Tigo Pesa anapaswa kujisajili na SportPesa, na kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kupitia huduma ya Tigo Pesa, kubashiri mechi anayoipenda na kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ili kujishindia zawadi za kila siku, wiki na hatimaye zawadi ya mwisho wa promosheni ambayo ni shilingi 15,888,000.

“Kumbuka mteja wa Tigo kupitia huduma ya Tigopesa anaweza kuweka pesa kwenye akaunti ya SportPesa kwa kupiga *150*01# au kupitia Tigo Pesa App.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa M-Pesa, kutoka Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, Kelvin Nyanda, alisema: "Kushiriki ni rahisi sana, kila mteja wa M-Pesa ana nafasi ya kushinda katika kipindi hiki kwa kuingia kwenye menyu ya malipo ya M-Pesa kisha chagua lipa bili, halafu michezo, kisha SportPesa, halafu fuata maelezo.

“Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wateja wetu kushiriki mara nyingi wawezavyo, maana ushindi upo kwa ajili yao sababu ya “Mshiko Deilee”, alihitimisha.

Habari Kubwa