SportPesa yamkabidhi Abdulaziz chake

10Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
SportPesa yamkabidhi Abdulaziz chake

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri SportPesa imemkabidhi rasmi mshindi wa awamu ya sita wa Jackpot, Abdulaziz Ibrahim (24), mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. milioni 521.4 ikiwa ishara ya kutimiza wajibu kama kampuni kwa washindi wake.

Baada ya mshindi huyo kutoka Sikonge mkoani Tabora kukabidhiwa zawadi yake alisema: “Nafurahi sana kwani baada ya kusubiri kwa kipindi kilichopangwa leo (jana) nimekabidhiwa rasmi fedha zangu.”

“Napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu kwa kuniongoza maana nilishajaribu mara kadhaa lakini sikufanikiwa.

“Siku niliyoshinda niliweka mikeka 10 na kila mmoja Sh. 2,000, katika mikeka yote 10 mkeka namba saba ndio niliofanikiwa kushinda kwa mechi zote, mimi ni shabiki mkubwa wa Manchester United na kwa hapa Tanzania nashabikia Young Africans. Siku niliyoweka mikeka yangu niliikosesha ushindi Man U ambayo ilikuwa inacheza na Leister City kupelekea kufanikisha vizuri ushindi wangu.

“Kwa upande wa SportPesa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Tarimba Abbas alianza kwa kuwashukuru waandishi wa habari kwa kuhudhuria tukio hilo muhimu la kumkabidhi mshindi mfano wa hundi ya Sh. milioni 521.4.

“Katika ushindi wake Abdulaziz ameweza kubaki na Sh. milioni 417.1 huku akitoa Sh. milioni 104.2 kama malipo ya kodi ya zuio.“

“Kila siku tunaendelea kuwa wabunifu ili kuhakikisha tunaboresha huduma na kuwafanya wateja wetu wazidi kufurahia kucheza na SportPesa,” alisema Tarimba.

Habari Kubwa