Stars mambo mazuri Afcon

01Jun 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Stars mambo mazuri Afcon

SHIRIKISHO la Soka Nchini (TFF), limesaini mkataba na Kampuni ya Romario Sports 2010 ya jijini Dar es Salaam, ili kupatiwa jezi kwa ajili ya timu zote za Taifa za hapa nchini.

Mkataba huo umekuja ikiwa ni siku moja kabla ya kikosi cha Timu ya Tanzania (Taifa Stars) kuanza maandalizi ya kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019) ambazo zitachezwa nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi 19 mwaka huu.

Rais wa TFF, Wallace Karia, alisema kuwa wanaishukuru kampuni hiyo ambayo watafanya nayo kazi kwa muda wa miaka mitatu na pia itakuwa inauza jezi za timu za Taifa na shirikisho hilo likipata sehemu ya fedha kutokana na mauzo hayo.

Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Minhaal Dewji, alisema kuwa huo ni mchango wao kwa taifa na watahakikisha kwa muda wote wanawapatia jezi zenye kiwango cha juu.

Dewji alisema kuwa kutokana na makubaliano hayo, sasa TFF itaanza kufaidika kutokana na mauzo ya jezi hizo.

Habari Kubwa