Stars na Zimbabwe kuonyeshwa live leo

13Nov 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Stars na Zimbabwe kuonyeshwa live leo

MCHEZO wa kirafiki wa kimataifa kati ya wenyeji, Zimbabwe na Tanzania utaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya taifa ya nchi hiyo (ZBC) leo kutoka mjini Harare.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas aliyeongozana na Taifa Stars nchini Zimbabwe, alisema jana kwamba timu ZBC nao wameipa haki Azam TV ya Tanzania kuonyesha pia mchezo pia.

"Kituo cha Televisheni ya Taifa hapa Zimbabwe (ZBC) na huko nyumbani wataungana na Kituo cha Televisheni cha Azam ( Azam Tv) inayopatikana kwenye king'amuzi cha Azam muda wote wa mchezo kuonyesha mchezo huo," alisema Alfred Lucas.

Taifa Stars itashuka kwenye Uwanja wa Taifa wa Harare kesho jioni kumenyana na wenyeji, Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Stars imefikia kwenye hoteli ya The Rainbow Towers mjini Harare na mchezo wa kesho utaanza Saa 9.00 Alasiri kwa saa za Zimbabwe, sawa na saa 10.00 jioni kwa saa za Tanzania.

Kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ni: Makipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na Aishi Manula, Mabeki ni Erasto Nyoni Michael Aidan, Mwinyi Haji, Mohamed Hussein na Vicent Andrew.

Viungo wa Kati ni Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Jonas Mkude na Muzamil Yassin na wale wa pembeni ni Shiza Kichuya, Simon Msuva na Jamal Mnyate na washambuliaji ni Ibrahim Hajib, John Bocco, Mbwana Samatta, Elius Maguli, Thomas Ulimwengu na Omar Mponda.

Habari Kubwa