Stars U-20 kuivaa Uganda leo

24Jul 2021
Saada Akida
Dar es Salaam
Nipashe
Stars U-20 kuivaa Uganda leo

TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 (U-23), inashuka dimbani leo kuivaa Uganda katika mchezo wa pili wa mashindano ya kombe la CECAFA kwa umri huo yanayoendelea nchini Ethiopia.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen, alisema amejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika michezo yote ya hatua ya makundi.

Alisema licha ya kutokuwa na maandalizi ya mapema, lakini wachezaji wamefanya vizuri katika mchezo wa kwanza wa hatua hiyo ya makundi kwa kuwafunga Jamhuari ya Kidemokrasia ya Congo.

Alisema tayari amefanyia kazi upungufu uliojitokeza katika mchezo wa kwanza na sasa kikosi kipo fiti kwa ajili ya mchezo wao huo dhidi ya Uganda.

Tanzania imepangwa kundi A pamoja na timu kutoka Uganda, Kenya na DR Congo.

Katika mchezo wa kwanza, Tanzania ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya DR Congo), bao hilo pekee likifungwa na mshambuliaji wa Namungo FC, Relliant Lusajo dakika ya 66.