Tanzania kuanza na Rwanda Challenge ya wanawake 2016

31Aug 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Tanzania kuanza na Rwanda Challenge ya wanawake 2016

TANZANIA imepangwa Kundi B pamoja na Ethiopia, Tanzania na Rwanda katika michuano ya ubingwa wa wanawake kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Nicholas Musonye

Tanzania itafungua dimba na Rwanda Septemba 12, kabla ya kucheza na Ethiopia Sept 16, wakati Nusu Fainali zitakuwa Septemba 18 na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na Fainali zitakuwa Septemba 20.

Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye aliwaambia Waandishi wa Habari juzi katika mkutano wa utambulisho wa Challenge hiyo ya wanawake mjini kampala, Jumatatu kwamba Uganda watakuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Katika sherehe za utambulisho wa michuano hiyo iliyofanyika makao makuu ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Musonye alisema nchi saba zimethibitisha kushiriki Challenge hiyo ya kwanza ya wanawake, itakayofanyika Jinja.

Mbali za Tanzania, Ethiopia na Rwanda ziliopo Kundi B, Kundi A linaundwa na timu za Uganda, Kenya, Burundi, na Zanzibar na michuano itaanza Septemba11 to 20, 2016.

Habari Kubwa