Tegete: Hali ni ngumu

09Mar 2016
Lasteck Alfred
Dar
Lete Raha
Tegete: Hali ni ngumu

LICHA ya kwamba wapo kwenye nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi wenye timu 16, Kocha wa Toto Africans ya Mwanza, John Tegete amedai kuwa ilipo timu yake kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu huu si sehemu salama hivyo atahakikisha anaboresha uwezo wa wachezaji wake ili kuweza kuinusuru timu.

Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na Kiongozi wa Timu ya Toto Africans ya Mwanza, John Tegete.

Tegete ambaye ni baba mzazi wa straika wa Mwadui, Jerry Tegete alisema, “ Kuwa kwenye nafasi ya tisa si salama kwani tunatofauti ya pointi 23 ambazo ni saba zaidi ya zile za wale wanaoshika mkia.

“Kuna haja yakuongeza nguvu kwa wachezaji wangu na kuwapa maarifa ya ziada ili kuepuka kushuka daraja. Tukipata pointi kama 12 tutakuwa kwenye nafasi nzuri na hatutaweza kushuka daraja.

Pointi 12 ina maana Toto African inahitajika kushinda mechi nne ili kujihakikishia nafasi ya kucheza msimu ujao.

“ Pointi 12 tutazipata kwa kucheza na timu zingine ambazo zipo na hali kama yetu hivyo hatuna shaka kuwa tutaweza kupata pointi hizo, zaidi tunahitaji wachezaji wetu wawe vizuri na tayari kwa mapambano,” alisema.

Habari Kubwa