TFF yaichongea Congo kuchezesha vijeba

22Sep 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
TFF yaichongea Congo kuchezesha vijeba

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema timu ya vijana ya Congo Brazzaville ilichezesha vijeba kwenye mechi dhidi ya vijana wa Tanzania – Serengeti Boys na kwa sababu hiyo, wamewasilisha malalamiko Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Katika mechi hiyo ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifaifa ya Afrika (U17) kwa vijana kwenye Uwanja wa Uhuru, Serengeti Boys ilishinda mabao 3-2.

Taarifa kutoka TFF zinaeleza kuwa wachezaji waliolalamikiwa ni Langa-Lesse Perce na Kiba- Konde Rodrique, ambao mbali na kutuhumiwa kuwa ni vijeba, pia walivalishwa jezi tofauti na walizovaa katika mchezo wao uliotanguliwa dhidi ya Namibia.

"Tayari rufaa imeshakwenda na imelipiwa," alisema kiongozi mmoja wa juu wa TFF (jina linahifadhiwa).
Kabla ya Tanzania kutuma rufaa hiyo, tayari Namibia iliwasilisha madai kama hayo, lakini walishindwa kusikilizwa kutokana na kushindwa kulipa ada kama taratibu zinavyoeleza.

Habari Kubwa