Tigo yanogesha East African Got Talent, kugawa mapesa

18Sep 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Tigo yanogesha East African Got Talent, kugawa mapesa
  • Wateja kujishindia zawadi za pesa taslimu hadi Sh mil. 7 na safari za kwenda kushuhudia onesho Kenya moja moja

MASHINDANO ya kusaka vipaji ya East African Got Talent yamezidi kunogeshwa baada ya Kampuni ya Tigo Tanzania, kutangaza ushirikiano na kutoa zawadi kwa wateja wake na watazamaji wa mashindano hayo kupitia promosheni ya EAGT Trivia.

Mtaalamu wa Kidigitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi akizungumza na waandishi wa habari kushoto ni Mratibu wa mradi wa EAGT, Redemptus Caesar.

Akizungumzia promosheni hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mtaalamu wa Kidigitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi, alisema, kupitia promosheni hiyo ya EAGT Trivia, wateja wa Tigo watakuwa na nafasi ya kushinda zawadi za pesa taslimu hadi kufikia sh. mil. 7. mbali na hiyo, wateja 40 watajishindia safari kwenda Kenya kutizama onesho moja kwa moja.

“Kama kampuni ya mapinduzi ya kidigitali, kila mara tunaagalia majukwaa na mianya ambapo tunaweza kuunganisha wateja wetu pamoja,” alisema

Alisema kuwa promosheni ya EAGT Trivia itatoa fursa sawa kwa wateja wetu kusimama pamoja kujishindia zawadi za pesa taslimu na kwenda kushuhudia onesho la moja kwa moja nchini Kenya katika mashindano hayo.

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi wa EAGT, Redemptus Caesar, alisema “Tuna furaha kuugana pamoja na Tigo mojawapo ya kampuni kubwa zinazoongoza kwa mawasiliano nchini Tanzania tunatarajia kuweka msingi thabiti kwa vijana wa Tanzania kuonesha vipaji vyao duniani,"

Hata hivyo Ngowi alifafanua kuwa wateja wa Tigo watakiwa kuchamgamkia fursa hiyo, huko akisisitiza kila mteja kujitokeza kushiriki.

Wateja wa Tigo wanaweza kujiunga na Trivia kwa kutuma neno 'TALENT' ’kwenda 5572’ au kutembelea http://tigoquizkitaa.co.tz. Baada ya kujiunga mteja atakuwa akijibu maswali yanayohusiana na EAGT, ili kujishindia zawadi mbalimbali za shindano hilo.

Habari Kubwa