Twiga Stars, U-17 zapaa na matumaini

01Nov 2020
Saada Akida
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Twiga Stars, U-17 zapaa na matumaini

KIKOSI cha Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), kimeondoka nchini leo na kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki mashindano ya COSAFA kikiwa na malengo ya kufanya vyema kwenye michuano hiyo.

Twiga Stars ni mwalikwa katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika kuanzia keshokutwa hadi Novemba 14, mwaka huu mjini Port Elizabeth.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime alisema kikosi chake kimejiandaa vizuri kuelekea katika mashindano hayo, na wanaamini wanakwenda kupambana na si kusindikiza.

Shime alisema mechi zote zitakuwa ngumu hasa kutokana na historia ya Twiga Stars inapokuwa kwenye michuano hiyo inayofanyika kila mwaka.

Kocha huyo alisema kikosi chake kinatarajia kutumia mashindano hayo kama sehemu ya maandalizi ya mechi yao ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za Vijana dhidi ya Senegal itakayofanyika baadaye mwaka huu.

"Mipango na mikakati yetu ni kuona tunafuzu kucheza fainali za dunia, tutatumia mashindano haya kujiimarisha na kuongeza uzoefu kwa wachezaji wangu, ila tutahakikisha tunaendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi katika kila mashindano tunayoshiriki," Shime alisema..........kwa habari zaidi fuatilia epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa