Twiga Stars waanika visingizio vyao

06Mar 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe Jumapili
Twiga Stars waanika visingizio vyao

TWIGA Stars - Timu ya Taifa ya Wanawake, imeanza vibaya safari ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka Zimbabwe katika mechi iliyochezwa mwishoni mwa wiki hii, lakini kocha Nasra Juma amesema hawajakata tamaa.

TWIGA STAR

Hata hivyo, Kocha wa Twiga Stars, Nasra Juma amesema kikosi chake bado kina nafasi ya kusonga mbele.
Akizungumza jana Nasra alisema kikosi chake kitakwenda kwenye mechi ya marudiano ikiwa na matumaini ya kushinda na kusonga mbele.

Alisema wana uwezo kuifunga Zimbabwe nyumbani kwao, hivyo hawaoni sababu ya kukata tamaa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza.

Nasra alisema kuumia nahodha wake, Sophia Mwasikili na kushindwa kuendelea kucheza kwa mshambuliaji, Shelder Boniface baada ya kuumia katika dakika ya 17, kuliharibu mipango ya ushindi.

Pia alisema kutowafahamu vizuri wapinzani wao ilikuwa moja ya sababu ya kushindwa kupata ushindi nyumbani.
Timu hizo zinatarajiwa kurudiana mjini Harare kati ya Machi 18-20 na mshindi atakutana na Zambia au Namibia.

Habari Kubwa