Twiga Stars yawafuata wanawake wa Cameroon

08Nov 2016
Faustine Feliciane
Dar es Salaam
Nipashe
Twiga Stars yawafuata wanawake wa Cameroon

KIKOSI cha timu ya Taifa ya wanawake 'Twiga Stars' kinaondoka leo kwenda Cameroon kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa Novemba 11, mwaka huu.

Kufuatia majukumu hayo ya Twiga Stars, Shirikisho la soka Tanzania (TFF), limesimamisha ligi ya Taifa ya Wanawake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema wiki hii utachezwa mchezo mmoja tu wa ligi na timu nyingine zitasubiri mpaka Twiga Stars itakaporudi.

"Ikumbukwe Twiga Stars inaenda Cameroon kutokana na mwaliko wa chama cha soka cha nchi hiyo..., mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa Cameroon inayojiandaa kushiriki mashindano ya kimataifa," alisema Lucas.

Kikosi hicho cha Twiga kinatajiwa kurejea nchini Novemba 13, mwaka huu.

Habari Kubwa