Uchaguzi TAFCA Ubungo Februari 18

17Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Uchaguzi TAFCA Ubungo Februari 18

MKUTANO Mkuu wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (Tafca) Mkoa wa Kisoka wa Kinondoni, utafanyika Februari 18, mwaka huu jijini Dar es Salaam katika ukumbi utakaotangazwa baadaye.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Tafca Kinondoni, Boniface Wambura alisema jana kuwa ajenda za kawaida za kikatiba
zitajadiliwa na kwamba mkutano huo utaoongozwa na Mwenyekiti wake, Eliutery Mholery, huku ukipanga tarehe ya uchaguzi ya kamati mpya ya utendaji baada ya iliyopo kumaliza muda wake.

Wambura alisema Mkutano huo utazungumzia uanzishaji wa Chama cha Makocha cha Wilaya mpya ya Ubungo ambayo imemegwa kutoka Wilaya ya Kinondoni.

Alisema Tayari Wilaya ya Ubungo imeshasajili na kufanya uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ubungo (Ufa).

Wambura ametoa wito kwa makocha wote wa Tafca Kinondoni kuhudhuria Mkutano huo muhimu kwa ustawi wao pamoja na mpira wa miguu kwa wilaya za Kinondoni na Ubungo.

Habari Kubwa