Usahihi habari kufuzu Olimpiki

17Jan 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Usahihi habari kufuzu Olimpiki

KATIKA ukurasa huu wa toleo letu la jana kwenye habari iliyobebwa na kichwa cha habari “Kufuzu Olimpiki kufanyika Misri” haikuwa sahihi.

Taarifa hiyo ambayo alinukuliwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kwanza ilipitwa na wakati, kwa kuwa awali ilitolewa rasmi Novemba mwaka jana.

Pia tunapenda kuweka usahihi kuwa mashindano ya kusaka timu za soka yatafanyika baadaye mwaka huu na timu ya Taifa ya Tanzania ya umri chini ya miaka 23 ilishatolewa.

Aidha, mkutano wa makatibu kutoka nchi za Jumuiya ya Madola utafanyika Aprili mwaka huu huko Zanzibar na si mwakani kama ilivyoandikwa hapo jana.

Tunaomba radhi kwa wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hii hususan TOC.