Uwanja wa Karume Mara kukarabatiwa

27Jun 2016
Na Mwandishi Wetu
Mara
Nipashe
Uwanja wa Karume Mara kukarabatiwa

KATIKA kuhakikisha timu zake zinafanya vizuri katika mashindano mbalimbali, uongozi mpya wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM) umesema kuwa utaufanyika matengenezo Uwanja wa Karume ili kufikia viwango vinavyokubalika hapa nchini.

Uwanja wa Karume Mara

Mwenyekiti wa FAM, Michael Wambura alisema chama hicho kimeshaanza mazungumzo na wamiliki wa uwanja huo ambao ni Chama cha Mapinduzi kwa ajili ya kupata baraka za kuanza ukarabati huo.

Wambura alisema lengo ni kuhakikisha uwanja huo unapitishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutumika kwa mechi za Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao ambapo timu yao ya Polisi Mara inatarajiwa kushiriki.

"Tunataka kuhakikisha uwanja unabadilika na kufikia sifa zilizowekwa na TFF, lengo ni kuzipa nafasi timu zetu kujiandaa vyema na mashindano mbalimbali, hasa Ligi Daraja la Kwanza," alisema Wambura, Katibu Mkuu wa zamani Chama cha Soka Tanzania (FAT sasa TFF).

Kiongozi huyo aliwataka wadau wa mkoa huo kujitokeza kushirikiana na uongozi mpya kusaidia maendeleo ya mchezo huo kwa kueleza kuwa maendeleo yatapatikana kwa nguvu ya pamoja ya Wana-Mara wote.

www.guardian.co.tz/circulation

Habari Kubwa