Wakala wa Yaya Toure, 
Guadiola wazidi kusutana

22Sep 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wakala wa Yaya Toure, 
Guadiola wazidi kusutana

Dimitri Seluk, wakala wa mchezaji Yaya Toure, amesema hatamuomba radhi kocha wa Manchester City, Pep Guardiola.


Seluk alitoa kauli ya kumponda Guardiola kufuatia uamuzi wa kocha huyo kutojumuisha jina la Toure kwenye kikosi cha timu hiyo michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Mapema juzi, Guardiola alisema hatampa nafasi Toure kwenye kikosi chake bila kwanza wakala wake kuomba radhi kutokana na kauli aliyoitoa.


Seluk alisema uamuzi wa kocha huyo raia wa Ufaransa kutojumuisha jina la Toure ni sawa na kumdhalilisha.
Seluk alisema: "Nini niombe…radhi? Guardiola ameshinda mechi kadhaa sasa anajiona kama mfalme. Naishi Ulaya, naweza kusema lolote nalotaka na Guardiola hawezi kunizuia.


"Sawa, nitaomba radhi kwa Guardiola, lakini awe wa kwanza pia kumuomba radhi Manuel Pellegrini kwa mabaya aliyomfanyia.

Kama yeye ni mstaarabu, mambo kama haya yanawezekana. "Guardiola pia lazima amuombe radhi Joe Hart. Haipendezi unakuja England kwa mara ya kwanza kisha unaanza kutibuana na wachezaji wenyeji.

Unapokwenda kwenye nchi ngeni, lazima uwaheshimu watu wa hapo na nchi yenyewe."
Toure amecheza mechi moja msimu huu akiwa na kikosi cha Man City.

Habari Kubwa