Wanawake Z'bar wajitosa riadha

05Jul 2019
Na Mwandishi Wetu
ZANZIBAR
Nipashe
Wanawake Z'bar wajitosa riadha

TOFAUTI na ilivyotarajiwa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, safari hii wanawake wengi wa Zanzibar wamehamasika na kushiriki katika mashindano ya riadha ya nusu marathon.

Katika mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki visiwani hapa, wanawake wengi wa rika tofauti walijitokeza na kushiriki mbio hizo za kilomita 21, 10 na tano zilizoanzia Ngome Kongwe na kuishia Chukwani kwa kilomita 21, Mazizini katika makutano ya barabara inayoelekea ZRB kwa kilomita 10 na kilomita tano zikiishia Kilimani Chini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Riadha Zanzibar (ZAAA), Muhidini Yasin, alisema wamefarijika kuona idadi kubwa ya wanawake kujitokeza na kushiriki na kwamba hatua hiyo inaonyesha dhahiri kwamba lengo lao la kuwahamasisha wanawake hasa wazawa kushiriki riadha kupitia mashindano hayo limefanikiwa.

"Tunashukuru ushiriki mkubwa wa wanawake kwa kilomita zote zilizoshirikisha mbio hizo, na huu ndio mwanzo mzuri wa malengo yetu,” alisema.

Katika mashindano hayo Pendo Pamba kutoka klabu ya mafunzo alishika nafasi ya kwanza kwenye kilomita 10, Rose Mary kutoka KMKM akashika nafasi ya pili na Catherina Bell kutoka Nungwi akaibuka mshindi wa tatu.

Kwa upande wa kilomita 21, Rosalia Fabian wa Klabu ya JKU aliibuka kidedea kwa kutumia muda wa saa 1:24.00