Washindi Bajaj SportPesa wanavyoboresha maisha

03Dec 2018
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Washindi Bajaj SportPesa wanavyoboresha maisha

Watanzania wameendelea kubadilisha maisha yao na kuwa ya juu kutokana na kujiongezea kipato kwa bajaj wanazoshinda kupitia Promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa, ambapo hadi kufikia leo jumla ya bajaj 74 zimekwenda kwa washindi.

Aidha, njia pekee na wewe kuweza kuwa miongoni mwa wanufaika walioboresha maisha yao, inaelezwa kuwa ni  rahisi sana kwani unachotakiwa kufanya ni kubashiri matokeo ya michezo kupitia SportPesa pekee.

Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba bado kuna bajaj 26 zimebaki kwa washindi wa michezo ya kubashiri kupitia SportPesa, na njia pekee ni kuanza kuweka ubashiri wako hivi sasa kupitia SportPesa.

Katika mahojiano maalum na Meneja Uhusiano wa SportPesa, Sabrina Msuya ameizungumzia promosheni hiyo inayoendelea hapa nchini, ambapo aligusia mambo makubwa manne.

 

Mwitikio wa promosheni

“Ni mkubwa tofauti na mwaka jana ambayo ilianza kutokana na mwitikio mkubwa wa Watanzania wengi kubashiri michezo mbalimbali kupitia SportPesa.

“Hivyo, kutokana na mwitikio huo mkubwa tumeona tuongeze zawadi nyingine tofauti na bajaj hizo tunazozitoa na lengo ni kuwanufaisha Watanzania.

 

Washindi sita kwenda Hispania, Uingereza

“Ni kati ya zawadi tutakazozitoa kupitia promosheni hii ya Shinda Zaidi na SportPesa, tofauti na bajaj tumepanga kutoa tiketi kwa washindi wetu kwenda kuangalia baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya Uingereza na Hispania.

“Tiketi tano ndiyo tulizopanga kuzitoa kwa washindi wetu, wakiwa huko SportPesa itawagharamia kila kitu ikiwamo chakula, malazi na usafiri wa ndani kwa kipindi chote.

“Washindi hao watasafiri kwenda kushuhudia ligi hizo Januari, mwakani baada ya promosheni hiyo kufikia kilele mwishoni mwa mwaka huu.

“Zawadi nyingine tuliyoiongeza ni ya jezi za Simba na Yanga na simu za smartphone ambazo zinaendelea kutolewa kila siku kwa washindi wetu wanaoweka ubashiri wao kupitia SportPesa."

 

Tofauti ya mwaka huu na mwaka jana

“Ipo kubwa na hilo limedhihirika kutokana na washindi kupatikana kutoka mikoa mipya na hiyo imeonyesha ni jinsi gani watu wengi wanabashiri kupitia SportPesa.

“Mwaka huu washindi wengi wametoka mikoa ya Mara, Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza, Kigoma na Tanga, lakini mwaka jana washindi wa bajaj walitoka Makambako, Newela, Arusha ambao ulitwaa bajaj zaidi ya 20.

 

Washindi waliopita walivyofaidika

“Kiukweli kabisa tunajivunia kama SportPesa, kwa kupitia promosheni hii tumefanikiwa kubadili maisha kwa Watanzania kupitia ushindi wao wa ubashiri wa matokeo.

“Mabadiliko yapo mengi kati ya hayo wapo wamenunua viwanja na wengine wamejenga nyumba kwa kupitia bajaj wanazoshinda kupitia promosheni hii inayoendelea.

“Wengine wanawalipia ada watoto zao ambao ndiyo jambo la msingi kuona watu wakiendelesha familia zao kupitia ubashiri wao."

 

Malengo yenu ni yapi?

“Ni kuona Watanzania wengi wakibadili maisha yao kupitia promosheni hii inayoendelea hapa nchini na kikubwa ni kuona wakifanya ujenzi wa nyumba, kununua viwanja na kuendeleza familia zao kupitia ushindi wa ubashiri wa matokeo kutoka SportPesa.

“Na hilo linawezekana kabisa, kikubwa wanachotakiwa kuanza kubashiri kuanzia leo na baada ya muda mchache wataona mabadiliko baada ya kushinda kupitia SportPesa."

 

Habari Kubwa