Yanga kuikabili Kengold kibabe

25Feb 2021
Saada Akida
Dar es Salaam
Nipashe
Yanga kuikabili Kengold kibabe

ILI kuhakikisha timu yao inasonga mbele, mabosi wa Yanga wamesema tayari wamepata taarifa muhimu za 'kuwamaliza' wapinzani wao katika mechi ya mzunguko wanne wa mashindano ya Kombe la FA, Kengold FC ya jijini Mbeya.

Yanga itawakaribisha Kengold katika mechi ya michuano hiyo itakayochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Thabit Kandoro alisema mchakato wa kuipeleleza Kengold ulianza mapema baada ya ratiba kutolewa na walimpatia taarifa hizo za kiufundi kocha wao, Cedric Kaze.

"Hatutadharau timu yoyote ambayo tunakutana nayo, Kengold FC sio timu ya kuibeza, tumewafuatilia na taarifa zao tumeziwasilisha kwenye benchi la ufundi ili kufanyiwa kazi," alisema Kandoro.

Kiongozi huyo aliongeza Yanga imejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi na kusonga mbele kwenye michuano hiyo ambayo bingwa wake atapata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Habari Kubwa