Yanga wamvuruga kocha APR

11Mar 2016
Lasteck Alfred
Kigali, Rwanda
Nipashe
Yanga wamvuruga kocha APR

AKIWA na wiki moja tangu alipopewa kibarua cha kuifundisha klabu ya APR ya Rwanda, Kocha Nizar Khanfi amesema haifahamu Yanga, hivyo atakachofanya ni kujaribu mbinu mbalimbali ili kuwamudu mabingwa hao wa Bara.

Kocha Nizar Khanfi.

Kocha huyo alisema ni vigumu kucheza na timu usiyoifahamu hata kidogo, lakini hali hiyo hatakuwa tatizo kubwa kwake.

“Ni ngumu kucheza dhidi ya timu usiyoifahamu, kabla ya kuja APR sikuwahi kuifahamu Yanga wala kufuatilia wanavyocheza.

“Silaha pekee niliyonayo ni mbinu mbinu zangu dhidi ya Yanga. Nilichokuwa nikikifanya kwa wachezaji wangu ni kuwapa mbinu mbalimbali.

Nimekaa na timu kwa
muda mfupi, lakini hiyo siyo sababu. Tutapambana na Yanga kwa staili watazokuwa wakicheza,” alisema kocha huyo raia wa Tunisia.

Nizar alisaini mkataba wa kuifundisha klabu APR mwishoni mwa wiki iliyopita na mchezo dhidi ya Yanga utakuwa wa kwanza kwake kesho.

Habari Kubwa