Yanga yachapwa baada ya miezi 23

03Jan 2018
Adam Fungamwango
Nipashe
Yanga yachapwa baada ya miezi 23

KIPIGO cha mabao 2-0 ilichokipata Yanga dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, kimeifanya timu hiyo kufungwa  idadi hiyo ya magoli kwa mara ya kwanza, baada ya miezi 23.

MBAO FC

Mara ya mwisho Yanga kupokea kipigo kama hicho cha mabao  ilikuwa ni Januari 30, mwaka 2016 dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani yaliyofungwa na Miraji Adam na Juma Mahadhi ambaye baada ya msimu huo, timu hiyo ilimsajili.

Kwa miezi yote hiyo, Yanga ilikuwa haipotezi mechi kwa idadi hiyo ya mabao zaidi ya 1-0 au 2-1.

Hata hivyo, rekodi hiyo imetibuliwa na Mbao FC kwa mabao ya Habib Kiyombo ambaye naye ameendeleza rekodi ya kuifunga timu hiyo.

Kwenye Ligi Kuu ya msimu uliopita, Kiyombo alifunga bao pekee kwenye mechi ambayo Mbao iliifunga Yanga bao 1-0 katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mei 20 mwaka huu.

Habari Kubwa