Yanga yaishangaa Simba

27Jun 2018
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Yanga yaishangaa Simba

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika, amesema hawashindani na timu yoyote kwenye usajili na amewashangaa Simba wanaodai wamewapiga 'bao' kwenye usajili wa baadhi ya wachezaji.

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika.

Nyika, aliliambia Nipashe kuwa wanaendelea na usajili wao na si kweli kuwa kamati hiyo ipo kimya katika mchakato huo.

Simba inatajwa kuwa katika hatua za mwisho kumsajili beki Pascal Wawa huku tayari ikiwa imemsajili mshambuliaji Adam Salamba ambao wote walikuwa wakiwaniwa na Yanga.

"Hakuna mchezaji ambaye tulikuwa tunamtaka au alikuwa kwenye mipango yetu, hao wanaotajwa upande wa pili, kamati inaendelea na usajili utofauti ni kwamba sisi mambo yetu tunayafanya kimya kimya mpaka yakamilike," alisema Nyika.

Alisema Wanayanga hawapaswi kuwa na hofu, wao kama viongozi wanaendelea na mambo yao na watakuwa na kikosi imara msimu ujao.

Mpaka sasa hakuna mchezaji mpya ambaye ametangazwa kusajiliwa Yanga msimu huu.

 

 

Habari Kubwa