Yanga yenye pointi tatu na KVZ zimetolewa nje katika michuano hiyo na kuzifanya timu za Azam FC na Malindi zilizokuwa kwenye Kundi B kusonga mbele.
Akizungumza na gazeti hili, Cannavaro, alisema kuwa vijana wake walijitahidi kucheza mpira mzuri na walikuwa na nia ya kupata ushindi lakini hawakutumia vyema nafasi walizozipata kutokana na kukosa uzoefu.
“Vijana wamejitahidi, japo kikosi chenyewe cha Yanga kipo Dar es salaam lakini hiki kilichopo kilikuwa kizuri, kimepambana hadi hatua waliyofikia mimi niseme haikuwa bahati yetu na mpira una matokeo matatu,” alisema Cannavaro.
Naye Kocha Mkuu wa Malindi, Salehe Mchupa, alisema lengo lao ni kuhakikisha wananyakuwa ubingwa wa mashiindano hayo mwaka huu kutokana na timu yake kujiandaa vyema na kuwa na uwezo huo.
"Mwaka huu tumejiandaa vizuri, tutaenda kuyafanyia kazi makosa madogo madogo tuliyoyaona katika mechi hii dhidi ya Yanga, hasa safu ya ushambuliaji ili kuhakikisha tunapata magoli mengi," alisema Mchopa.